Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea kuhusu vigezo vinavyotumika na serikali kuwanyima mkopo wanafunzi waliosoma shule za binafsi, huku akieleza kuwa sera ya elimu imefanya ubaguzi.
"Tunachoangalia ni nani mwenye uhitaji zaidi, sio suala la kibaguzi, bajeti ni iliyopo ndogo wahitaji ni wengi. Kwa wanafunzi waliopata bahati ya kusomeshwa na wafadhili shule binafsi serikali haiwanyimi mikopo tutahitaji ushahidi kweli walifadhiliwa". - William Ole Nash
Aidha Mhe. Ole Nasha ameongeza "Kuhusu watoto ambao wamesoma shule binafsi kutoruhusiwa kupata mikopo ni suala la kuangalia kati ya mtu ambaye ameweza kulipa milioni 3 au 4 ya shule ya msingi na sekondari na yule ambaye hakuweza, ni yupi utampa kipaumbele kupata mkopo, sio tunabagua".- William Ole Nasha