Serikali Yakiri Ubovu Mashine Za EFD

Serikali Yakiri Ubovu Mashine Za EFD
Serikali imesema mashine za kielektroniki za (EFD) hazifanyi kazi kwa sasa nchi nzima ambapo imesambaza wataalamu nchi nzima kutatua ttaizo hilo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu mwongozo wa spika ulioombwa na Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa aliyetaka kujua serikali imejipangaje kwa kuwa uharibifu wa mashine hizo unalipotezea taifa mapato na kwamba linaweza kuwa ni tatizo lililotengenezwa na baadhi ya watu kwa ajili ya kuhujumu mapato ya serikali.

Akijibu swali hilo Dk. Kijaji amesema mashine hizo zilianza kutofanya kazi kuanzia Mei 11, mwaka huu na baadaye likatatuliwa.

“Wiki moja baada ya kutatuliwa tatizo likajirudia hadi leo, lakini serikali imepeleka wataalamu wa ICT katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa ajili ya kutatua tatizo hilo ambalo naamini litatatuliwa ndani ya muda mfupi ujao,” amesema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad