Serikali yasema aihusiki na Taasisi inayowatoza fedha Wanawake kupitia jina la Mama Samia


Serikali kupitia Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Muhagama imesema aihusiki na Taasisi inayowatoza wanawake sh. elfu kumi kumi kupitia jina la Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu katika mkoa wa Kigoma.

Akijibu swali la Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Kigoma,Josephine Gezebuke aliyehoji,

Katika Mkoa wa Kigoma iko NGO’s ambayo imezunguka kwa muda wa wiki mbili katika wilaya zote saba ikiwatoka wanawake sh. elfu 10, 10 na kuwapigisha picha na kuwaahidi kwamba serikali itatoa mikopo kwa kupitia mfuko wa Makamu wa Rais, Mama Samia, Je? ninataka serikali inieleze mpango huo wa kutoa pesa kupitia mfuko wa Mama Samia upo?

“Shughuli zote za uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi katika nchi yetu ya Tanzania zinasimamiwa na sera 2004 na sheria ya uwezeshaji wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004 ambayo inaruhusu uanzishwaji wa Taasisi mbalimbali kisheria, Taarifa kuhusu Taasisi hiyo zilishapatikana ndani ya serikali na ofisi ya Makamu wa Rais ilishatoa tamko la kuikana taasisi hiyo kwamba haihusiki nayo,” amesema Waziri Jenista.

“Ninaomba nichukue nafasi hii kuuagiza uongozi wa Mkoa wa Kigoma kuifuatilia taaisi hiyo na kuikana na kuipa maelekezo kwamba ofisi ya Makamu wa Rais aihusiki na jambo hilo na kama wanaendesha shughuli hizo kwa kutumia sheria taratibu nyingine wanapaswa kujieleza kwa kutumia sheria na taratibu zingine walizozifauta lakini sio ofisi wa Makamu wa Rais.”

Aidha Jenista amesema kuwa kama Taasisi hiyo itaendelea kuwadanganya wananchi kutumia mgongo wa Ofisi ya Makamu wa Rais serikali haitasika kuchukua hatua kali.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad