Nchini Kenya kumekuwa na mjadala mkubwa juu ya ugavi wa mali pindi wanafamilia wanapopeana talaka, jambo kubwa likiwa ni iwapo wanandoa wanatakiwa kugawana mali nusu kwa nusu wanapoachana kwa talaka au la?.
Jaji wa mahakama kuu nchini humo John Mativo amepinga wanandoa kugawana mali nusu kwa nusu wanapo achana kwa talaka uamuzi ambao wengi wameuchukulia kama pigo kwa haki za wanawake.
Uamuzi huo umetokana na sheria ya ndoa nchini humo ambayo hata hivyo imekuwa ikipingwa na shirikisho la mawakili wanawake Kenya FIDA wakidai kuwa sheria hiyo inawanyanyasa wanawake.
Ombi la FIDA limekataliwa na mahakama kwa madai kuwa kuruhusu kugawana mali nusu kwa nusu kutatoa mwanya kwa watu kuingia katika ndoa kwa lengo la kujinufaisha.
Mahakama imesema sheria haiwanyanyasi wanawake kwasababu umauzi huu pia utakuwa na manufaa na kuwalinda wale wanaofanya kazi kwa bidii katika familia.
Sheria Yawabana Wanandoa Kenya, Hakuna Kugawana 50/50 Mkiachana
May 15, 2018
Tags