Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Nikki wa Pili amesema ili wasanii watambulike kama wafanyakazi ni lazima serikali itambue wasanii wanafaje kazi na iwapo wanataka kuilinda ijue inalinda kitu gani.
Amesema baada hapo kinaweza kuanzishwa chama cha wasanii wafanyakazi ambacho kinasimama na kutengeneza kanuni na taratibu za mfanyakazi huyo na kitu hicho kutafsiriwa kama sheria.
“Kubadilisha sanaa kuwa biashara hicho ni kitu kingine, so niwajibu wa msanii kujifunza misingi ya biashara, hiki nilichonacho mkononi ninawezaje kukiuza? . Ukinipa uwaziri kitu cha kwanza ni kufanya utafiti mkubwa wa biashara ya muziki,” amesema.
“Kujua hii biashara inafanyikaje, uhalisia wake ni upi na huo uhalisia wake umetengeneza picha gani, then kutoka hapo tunawezaje kwenda mbele, bila kutafiti kwa facts utapiga bla! bla!,” Nikki wa Pili amesema hayo katika mahojiano na JJ wa Jembe FM.
Nikki wa Pili kutoka kundi la Weusi kwa sasa anatamba na ngoma Hesabu ambayo amemshirikisha producer, S2kizzy.