'Sikutosheka Kushiriki Ngono Mara 5 kwa Siku'

'Sikutosheka Kushiriki Ngono Mara 5 kwa Siku'
Shirika la wahisani la Relationship charity Relate limetoa wito kwa watu walio na uraibu wa ngono kupata usaidizi nchini Uingereza. Waathiriwa wawili wanazungumzia kuhusu athari za kuwa na pepo la ngono.

''Mara nyengine hata kushiriki ngono mara tano kwa siku haikutosha''.

Mama wa watoto 3 Rebecca Barker anasema kuwa tatizo hilo lilitawala maisha yake 2014 na kuvunja uhusiano wake

"Ilikuwa kitu cha kwanza kuja katika fikra zangu wakati nilipoamka , sikuweza kuitoa katika fikra zangu'' , alisema mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 37 kutoka eneo la Tadcaster Kaskazini mwa Yorkshire.

"Nilihisi kana kwamba kila kitu kilikuwa kikinikumbusha kuhusu tendo la ngono. Nadhani ilitokana na shinikizo la mawazo . Nilihisi kwamba mwili wangu wote ulikuwa ukitamani kushiriki katika shughuli hiyo.

"Ilikuwa ikinigonga na dakika tano baadaye niliitaka kushiriki tena tendo la ngono.

Nilihisi upweke, nilisalia nyumbani kwa sababu nilihisi aibu, nilikuwa nikifikiria kufanya ngono kila wakati. Hata iwapo hakuna mtu ambaye angeweza kugundua kilichokuwa katika fikra zangu , nilihisi vibaya kuwa karibu na watu wengine.

Ms Barker alivunja uhusiano wak na mpenziwe na kubadilisha maisha yake ili kutibu pepo wa ngono.
Pepo la ngono la Bi Barker lilizua matatizo makubwa katika uhusiano wake, ijapokuwa mpenziwe alipendelea hali yake kwa mara ya kwanza lakini alishindwa kuidhibiti.

"Mara ya kwanza alikuwa akifurahia lakini mwisho mwisho hakuweza kuelewa na baada ya miezi michache alianza kuuliza maswali ni wapi hisia hizo zilikuwa zikitoka .

"Alinishutumu kwa kuwa na uhusiano wa nje- alidhani kwamba nilikuwa nikihisi kufanya makosa ndiposa nikataka kushiriki naye tendo la ngono.

Uhusiaono wake ulivunjika
Mnamo mwezi Novemba 2014, bi Barker "alitaka kupumzika kutoka katika uhusiano huo na alienda kuishi na mamake.

"Nilipoondoka nilimwambia mpenzi wangu kwamba nilihitaji kuimarika kitabia na hisia. Alinikubali kuondoka na uhusiano wetu ukaisha polepole''

"Nilikuwa chini ya uangalizi wa mtaalamu wa matatizo ya kiakili wakati huo-ambaye alikuwa akinimbia kwamba atabadilisha dawa zangu , lakini hakusema kwamba kulikuwa na makundi ya usaidizi.

Bi Barker alipatikana na shinikizo la kiakili 2012 baada ya kujifungua mwanawe wa tatu. Alisema kwamba alibadilisha kazi aliyokuwa akifanya , akakosana na mpenzi wake na kuhamia Ufaransa.

''Nilifanya mabadiliko katika maisha yangu ili kukabiliana na shinikizo hilo la mawazo na pepo huyo wa ngono na ni hatua hiyo ilionisaidia'', alisema.

Relate inaelezea uraibu wa ngono kuwa kushiriki ngono isioweza kudhibitika na shirika la afya duniani WHO linatarajiwa kuweka tatizo hilo miongoni mwa matatizo ya kingono katika orodha yake ya kitaifa ya magonjwa (ICD) mnamo mwezi Mei 2019.

Graham, ambaye jina lake limebadilishwa anasema kuwa tatizo lake la kuwa na pepo wa ngono lilimlazimu kulala nje na mamia ya makahaba na kumfanya kuwa na hatia kubwa.

Wakati unapokuwa na pepo huyo unakuwa ukifikiria kitendo hicho mara kwa mara kutoka wakati unapoamka hadi wakati unapoenda kulala. Haikuwa hali nzuri, wakati unapoamka alfajiri na kutumia dawa za kukabiliana na magonjwa ya zinaa .

Bi Barker amesema kuwa ngono nio kilichokuwa kitu cha kwanza katika mafikira yake
Alikuwa na uhusiano na makahaba 3
Graham, ambaye yuko katika miaka yake ya 60 anakadiria kwamba alilipa mamia ya paundi kwa mwezi kwa miaka kadhaa ili kuimarisha uhusiano wake na baadhi ya makahaba

"Uhusiano ulioanza kama urafiki kazini ulichochea mwengine -lakini kama mahusiano ya afisi ambayo yangeanza kutokana na mhusika mmoja kutokuwa na raha katika ndoa yake tatizo langu lilikuwa pepo wa ngono ambaye nililazimika kumpatia mahitaji yake kila siku.

Una uhusiano mmoja na baadaye unataka mwengine na baadaye unajiingiza katika mwengine. Na baadaye niligundua kwamba hatua mojawapo ya haraka ya kukabiliana na tatzio langu ni kulipia huduma hiyo .

Nilikuwa nikishiriki ngono na makahaba mara tatu ama hata nne kwa wiki.

Ni sawa na kuwa mlevi , ni tatizo linalokujia katika akili yako-Unahisi na kupanda hisia unapolifikiria na unapolitenda katika mipango yako na baadaye unapomaliza unajiambia kwamba hutawahi kufanya tena.

Graham alisita kuendelea na maisha hayo ya kutisha wakati mkewe alipopata barua pepe na kumshutumu.

Alitafuta usaidizi kwa mashirika yanayowasaidia watu wa tatizo lake nchini Uingereza kama vile Sex Addicts Anonymous (SAA), shirika ambalo lina makundi 78 nchini Uingereza na kwamba amewacha kujihusisha na ngono nje ya ndoa yake kwa miaka kadhaa.

Wakati nilipohudumiwa nakumbuka kuhisi kumshukuru Mungu- na kusema kitu kitabadilika .

Nileinda kwa shirikja hilo kwa tiba ya kuwacha kushiriki katika ngono za nje ya ndoa.

Nahisi afueni kulekea katika mikutano hiyo na kuona watu ambao wako katika hali mbaya zaidi ya nilivyokuwa. Kwa watu walio katika tatizo hili nataka wajue kwamba kuna njia nyengine na unaweza kujiondoa katika tatizo hilo.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad