Siri Yavuja Baada ya Harusi ya Mwanamfalme Kufanyia ‘Honey Moon’ Afrika, Nchi Mbili Zatajwa

Siri Yavuja Baada ya Harusi ya Mwanamfalme Kufanyia ‘Honey Moon’ Afrika, Nchi Mbili Zatajwa
Ikiwa ni siku moja imepita tangu harusi ya kihistoria ya kifalme ifanyike nchini Uingereza, kati ya Prince Harry na Meghan Markle sasa maswali mengi yanakuja ni wapi wanandoa hao watakwenda kwa ajili ya fungate (Honey Moon).

Kwa mujibu wa mtandao wa Travel + Leisure umeeleza kuwa wawili hao huenda wakaja Afrika kwa ajili ya fungate na nchi zilizotajwa ni Namibia na Botswana.

Hata hivyo, vyanzo vingi vya habari vinaitaja nchi ya Namibia kuwa ndiyo itakuwa sehemu ya kwanza kwa wawili hao kupumzika kwa ajili ya fungate.

Mwaka 2017 kwenye birthday ya Meghan, wawili hao walienda nchini Botswana kwa ajili ya kusherehekea siku hiyo ya mfanano wa kuzaliwa.

Kwa mujibu wa mtandao wa jarida la Vogue, bajeti ya Honey Moon kwa wawili hao ni Dola $221,175 sawa na tsh milioni 505.

Wawili hao kabla ya kuanza fungate wanatarajiwa kwenda nchini Mexico kumuona baba mzazi wa Meghan, Thomas Markle (75) ambaye hakuhudhuria kwenye harusi kutokana na maradhi ya moyo yanayomsumbua kwa muda mrefu.


Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Weee. MwNdishi sio Mecico nchi sio Mexico yule ni Mmarelani. Na hiyo ni mexico ya Marekani kitongiji cha Tijuana.Ila ndio haiko mbali na Mexico border ili uwingingie Mexico nchi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad