Spika Ndugai: Wizara Ya Fedha Ijitathmini

Spika wa Bunge, Job Ndugai ameitaka Wizara ya Fedha na Mipango, ijitathmini baada kushindwa kupeleka kwa wakulima wa korosho fedha za tozo za mauzo ya nje ya zao hilo.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo Mei 24, amesema kinachofanywa na wizara hiyo hakiwezi kukubaliwa kwa sababu kinaathiri zao la korosho nchini alipokuwa akijibu mwongozo wa kutaka kuahirisha bunge ulioombwa na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) aliyetaka bunge lisitishe shughuli zake na kujadili suala la serikali kutotoa fedha hizo kwa wakulima wa korosho.

Nape amesema: “kutopelekwa fedha hizo kumesababisha bei ya mbolea aina ya sulphur kupanda kutoka Sh 16,000 hadi 75,000”.

Akiunga mkono hoja hiyo Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) amesema kutopelekwa kwa fedha hizo kunatokana na utaratibu wa serikali ya awamu ya tano kutofuata sheria zinazopitishwa na bunge.

Akijibu miongozo hiyo, Spika Ndugai amesema suala hilo liachwe ili alifikishe kwa Waziri Mkuu kwa hatua zaidi.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Hawa Ghasia amesema hatua zilizochukuliwa na kamati yake juu ya hoja hiyo ya Nape.

Lakini pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri , Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama alisema hoja hiyo ya Nape inahitaji mjadala zaidi ingawa serikali imeshatoa Sh bilioni 10 kwa ajili ya zao la korosho.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad