Bongo5, Michuzi pamoja na Lemutuz ni moja kati ya Blogs na Online TV ambazo zimekabidhiwa leseni ya kufanya huduma hizo huku baadhi ya blogs kama Muungwana,Dar24, Millardayo, 8020 Fashion na Mwanaharakati Mzalendo na nyingine nyingi zikipewa leseni ya kurusha matangazo kupitia blogs pekee.
Akizungumza Ijumaa hii na waandishi wa habari na Wanablogs katika ukumbi wa TCRA, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba alisema zoezi hilo endelevu lina lengo la kuzuia uanzishwaji holela wa blogs na online tv ambao unaweza kusababisha madhara kwa jamii.
“Jambo la kwaza tunazuia uanzishwaji holela wa vyombo vya habari mtandaoni usiokidhi viwango vinavyotakiwa, ikumbukwe kwamba umiliki wa vyombo vya habari bila tozo unaweza ukaleta utitiri wa vyombo hivi na ikawa changamoto katika usimamizi na kwa jamii,” alisema Mhandisi James Kulaba.
Aliongeza, “Jambo la pili ni kuleta ushindani sawa,itakuwa sio vyema vyombo vya habari vinavyotumia majukwaa mengine kulipia leseni wakati vyombo vya mtandaoni havilipii gharama yoyote. Na jambo la tatu ni kutambua watu wenye nia safi ya kutoa huduma hii ya maudhui mtandaoni kwa jamii yetu,”
Mhandisi James amezitaka online tv pamoja na blogs mbalimbali kuendelea kujitokeza ili waweze kujisajili na kufanya kazi kwa uhuru huku akidai hatua hiyo itafungua milango ya kibiashara kwa blog na online tv.
VIDEO: