Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeitaka klabu ya Yanga kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi za viongozi wake waliojiuzulu ikiwemo ya Mwenyekiti kwa wakati kwani tayari muda umeshapita.
Agizo hilo limetolewa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF Revocatus Kuuli na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Herman Julius akimtaka kuhakikisha klabu ya Yanga na nyingine zinafanya uchaguzi haraka iwezekanvyo.
Mbali na Yanga klabu nyingine zinazotakiwa kufanya uchaguzi kwasasa ni AFC ya Arusha ambayo inashiriki Ligi daraja la kwanza na Coastal Union ya Tanga ambayo imerejea ligi kuu msimu huu.
Yanga imekuwa chini ya Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti, Yussuf Manji Mei mwaka jana ambapo imetimiza mwaka saa ikiwa bila Mwenyekiti.
Tayari klabu ya Yanga imeshatangaza kufanya mkutano mkuu wa wanachama mwezi ujao na huenda moja ya agenda katika mkutano huo zinaweza kuwa ni uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakaoipatia viongozi wapya.