TIMU ya Yanga Hoi Kwa Waarabu...Yachapwa 4 Bila

Wawakilishi wa Tanzania katika kombe la  shirikisho Afrika (Caf Confederation Cup) Yanga wameanza vibaya hatua ya makundi baada ya kufungwa mabao 4-0 kwenye mchezo wao wa kwanza wa makundi dhidi ya USM Alger ya Algeria.

Yanga ikicheza ugenini bila nyota wake wengi wa kikosi cha kwanza ilianza kuruhusu goli la kwanza dakika ya nne lakini hadi kipindi cha kwanza kina malizika Yanga ilikuwa nyuma kwa magoli 2-0.

Kipindi cha pili Yanga ikaruhusu tena goli la mapema ndani ya dakika 10 za kwanza na kuifanya USM Alger kuongoza kwa magoli 3-0, wakati mchezo ukiwa kwenye muda wa nyongeza beki wa Yanga Andrew Vicent alimfanyia madhdambi mchezaji wa USMA na mwamuzi kuamuru ipigwe penati ambapo golikipa wa USM Alger aliifungia timu yake goli la nne.

Matokeo ya mechi nyingine za Kundi D, Rayon Sports imetola sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya. Kwa maana hiyo, USM Alger inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi tatu ikifuatiwa  na Gor Mahia pamoja na Rayon Sports zenye poini mojamoja baada ya kila timu kucheza mechi moja.


Tags

Top Post Ad

Below Post Ad