Trump Atilia Shaka Mkutano Adimu na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un

Trump Atilia Shaka Mkutano Adimu na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un
Rais Trump ametilia shaka kufanyika mkutano adimu na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un mwezi june huko Singapore .

Amesisitiza kuwa hata hivyo Korea kaskazini itapaswa kutimiza vigezo vilivyowekwa ambayo ni nadra kutokea.

Korea Kaskazini ilikwisha sema kuwa inaweza kujiondoa katika mkutano huo iwapo Marekani inasisitiza suala la kuachana na mpango wa silaha za nyuklia.

Rais Trump amezungumzia mkutano huo,mara baada ya kumpokea katika ikulu ya Marekani rais wa Korea Kusini Moon Jae-in.


Hata hivyo rais trump hakuweka wazi ni masharti gani ambayo yamewekwa kwaajili ya mkutano huo,na alipoulizwa na waandishi wa habari juu ya masharti aliyiwekea Korea Kaskazini amesema kuwa suala la kuachana na silaha za nyuklia ni lazima litekekelzwe na Korea Kaskazini.

Rais wa Korea Kaskazini kukutana na mwenzake wa Kusini
Korea Kaskazini kufunga eneo la kufanyia majaribio ya nyuklia Mei
Mkutano huo kati ya rais Trump na Kim Jon-un uanatarajiwa kufanyikwa June 12 nchini Singapore ukitanguliwa na mkutano wa marais wa Korea hizi mbali uliofanyika mwezi April.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad