Ukipoteza Passport Mpya ili Kuipata Nyingine Utalipa Shilingi Laki Tano


Kamishna wa Uhamiaji, Uraia na Pasipoti, Gerald Kihinga amesema Mtanzania atakayepoteza hati ya kielekroniki ya kusafiria inayopatikana kwa Tsh. 150,000 atalazimika kulipa Tsh. 500,000 kupata mpya

Pia aliongeza kuwa iwapo ataipoteza tena hiyo aliyoipata kwa Tsh. 500,000 basi atalipa Tsh. 750,000 ili aweze kupata nyingine

Aliyasema hayo jana katika uzinduzi wa utoaji wa hati hizo ambapo tayari hati 15,101 zimeshatolewa kwa Watanzania tangu kuanza kwa utoaji huo Januari mwaka huu.

Kihinga amesema zipo kesi nyingi za watu kupoteza hati zao za kusafiria na baadhi yake ni zile zinazotokea katika matukio yasiyohitaji uwapo wake hati hizo hivyo gharama hiyo itasaidia watu kutunza hati zao
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad