Upinzani Burundi Wacharuka...Wakataa Matokeo ya Kura ya Maoni

Muunganano wa upinzani nchini Burundi Amizero y'Abarundi umetangaza kuwa hautambui matokeo ya kura ya maoni, iliyofanyika siku ya Alhamisi ili kuibaidilisha Katiba ya nchi hiyo.

Kiongozi wa muungano huo Agathon Rwasa amesema kura hiyo ya maoni haikuwa huru na haki.

Aidha, ameongeza kuwa demokrasia haikushuhudiwa katika zoezi hilo la Alhamisi.

Rais Pierre Nkurunziza anatarajiwa kuwania urais mwaka 2020, na kusalia madarakani hadi mwaka 2034.

Kauli hii ya muungano huo wa Amizero y'Abarundi uliokuwa unapinga mabadiliko ya katiba, imekuja wakati huu Tume ya Uchaguzi ikitarajiwa kutangaza matokeo ya mwisho.

Matokeo ya awali kutoka mikoa 17 kati ya 18 ya nchini humo, yanaonesha kuwa kura ya ndio imepata ushindi wa kati ya asilimilia 50 na 85.

Kuelekea siku ya kupiga kura, wanasiasa wa upinzani walilalamika kutishwa na wengine kufungwa jela.

Siku ya Ijumaa Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Human Rights Watch, lilitoa ripoti iliyoshtumu maafisa wa usalama na vijana wa kundi la chama tawala Imbonerakure kuwatishia, kuwapiga na hata kuwabaka wapinzani wa serikali, madai ambayo serikali ya Bujumbura imekanusha.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad