Ushauri: Mama Mkwe na Ndugu zake Wamepanga Waje Kwangu Kunihoji Kwanini Sifungi ndoa

Habari wakubwa;
Mimi naishi na mwanamke miaka 5 sasa sijafunga nae ndoa, Tumebahatika kupata mtoto mmoja ambaye kwa sasa ana miaka 4, mimba ambayo nilimtia punde tu baada ya kumaliza chuo;
bahati mbaya nilipomaliza chuo sikubahatika kupata ajira, nikawa naishi kwa kufanya vibarua elfu 50 kwa week, wakati nikifanya vibarua hivyo nikiwa naishi nae, aliniambia japo nikajitambulishe kwao, sikuwa na kipingamizi nikaapeleka barua ya uchumba, nikajibiwa pamoja na kupewa kiwango cha posa ambacho sijafanikiwa kukilipa hadi Leo.

SABABU ZINAZONIKWAMISHA NISIFUNGE NDOA
Katika history nakumbuka Wakati tukiwa chuo, Mimi nikiwa dar na yeye akiwa mkoani, yeye alikuwa anapokea bumu kubwa kuriko Mimi, lakini kila changamoto aliyopata kwa kidogo nilichonacho nilimrushie yeye punde tu aliponililia shida,
Mimi kila nilipokumbana na shida nilipokuwa nampigia kusema ukweli alikuwa mgumu sana, na hata anapofikia kutoa alinipa huku akisema sema maneno, nilivumilia, lakini ilikuwa inaniuma sana vile nilivyotumia nguvu kubwa kupata msaada wake, wakati Mimi akipatwa na shida nilikuwa tayar kushinda njaa ili nimtumie yeye!..

Nakumbuka siku moja nilimuomba aniazime elfu 10 ya kula, akaniambia hana, Mungu si athumani jioni yake akanipigia simu kwamba yuko polisi kuriport kaibiwa laki mbili mchana, aliniambia hivyo huku tayari akiwa amesahau kwamba nilimuomba hela ya kula anitumie akaniambia hana hela.........Nyway HAYO YOTE YA NYAKATI ZA CHUO NILISAMEHE NIKAJUA NI DHIKI ZA CHUONI TU ATABADILIKA.

Tukiwa tunaishi nae, kuna kikazi kilipatikana nikamuunganishia akapata, bahati mbaya wakati akiwa anaendelea na kazi Mimi kibarua kikasimama,
akiwa na ile kazi kiila nikimpgia simu alikuwa busy sana, yaan hata akisema subiri kidogo nitakupigia, wala hakupiga, na kwangu akahama akaenda kuishi kwa mama yake,
hata kodi ya nyumba ilivyoisha alinijibu majibu ya ajabu sana....anyway nisiseme sana lakini mwisho Wa siku nilihangaikaa wee nikafanikiwa kuendeleza maisha kivingine lakini mamamkwe wala hakunitetea,

Baada ya kupata kazi , niliendesha maisha yangu vizuri, aliposikia nimepata kazi akaanza kuja kunisalimia kwa kisingizio cha kufuata hela ya matumizi ya mtoto, Mara anakuja analala, Mara akasema kule anapokaa kwa mama yake pamebana kwahiyo akaamua kurudi, akawa anapika na kupakua; Baada ya Muda akaanza kuniuliza ndoa tunafunga lini! Nikamjibu sipo tayari kwa sasa,
Hali hii imeendelea hivohivo, Akaniuliza kwanini tunaishi pamoja? nimekuwa nikimjibu Arudi kwao hadi nitakapokuwa tayari nitamfuata,

Kwanza kabisa akipanga lake au kuondoka hata usipompa ruhusa yeye huwa anatoka, kiufupi huwa ananipa taarifa siyo kuomba ruhusa; Siku alikwenda kwa mama yake nikampigia simu mama yake kumuuliza kwanini binti yake kaondoka bila kuaga? Mama Mkwe alinijibu kwamba wewe si unamkataza asije kusalimia kwao!...nikamjibu mamamkwe Basi akae huko huko asirudi;
Baada ya siku mbili akawa karudi, sikumfukuza nikamuacha;
Kiila siku ananiuliza ndoa lini? na Mimi namjibu, Unataka Hayo matatizo yako niyafungie ndoa? Nikamwambia waambie hao ndugu zako wanaokutuma kwamba; Tabia yako haijanivutia kufunga ndoa;

Tangu nimjibu hivo Mama yake anataka twende anataka tuongee, kutokana na hasira zangu, nilimwambia binti yake amwambie sitaenda,
Baada ya kuambiwa hivo, MAMAMKWE KESHO JUMAPILI WAMEKUBALIANA KUVIZIA MIMI NISIPOTOKA WAJE KUZUNGUMZIA SUALA LA NDOA!

Je; Niwaambie laivu kwamba tabia ya binti yao haijanivutia? au nitumie lugha ya kistaarabu niseme bado najipanga?
maana hadi napata hofu maana ndo kwanza nimemaliza kujenga nyumba mbona wanaforce ndoa?
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad