Video ya ‘Mvumo wa Radi’ ya Alikiba yafanyiwa zengwe YouTube, mwenyewe atoa tamko

Video ya wimbo wa ‘Mvumo wa Radi’ ya Msanii wa Bongo Fleva, Alikiba imeelezwa kuwa imefanyiwa figisu figisu hususani kwenye suala la Watazamaji (Views) kwa kile kilichoelezwa kuwa hawaongezeki toka itoke video hiyo siku ya Ijumaa.

Alikiba amesema amepokea malalamiko hayo na hata hao wenyewe wamelitambua tatizo hilo na tayari wametuma malalamiko hayo makao makuu ya YouTube Afrika kuweza kutatua changamoto hiyo, na kuwaomba mashabiki wake waendelee kutazama kichupa hicho.

“Tunafahamu tatizo la kutokuongezeka kwa views kwenye akaunti ya YouTube ya ALIKIBA, na tupo kwenye mawasiliano ya moja kwa moja na makao makuu ya YouTube Africa ambao wanafanya kila jitihada kutatua tatizo hili kwa haraka iwezekanavyo. Shukrani kwa uvumilivu wenu na support mnayoendelea kutupa! Endeleeni kuangalia video ya Mvumo wa Radi,“ameeleza Alikiba kwenye taarifa yake kwa umma.

Video ya Mvumo wa Radi tangu jana Mei 12, 2018 imekuwa namba moja kwenye Trending ya video zinazotazamwa zaidi Tanzania na mpaka sasa bado ipo namba moja lakini tangu jana licha ya kuwa namba moja bado views wanaongezeka taratibu sana ukilinganisha na siku ya Ijumaa.

Kwa siku ya Jana hadi leo wameongezeka watazamaji chini ya 70+k ile hali kwa siku ya Ijumaa hadi Jana Jumamosi video hiyo ilikuwa imetazamwa na watu 690+k .

Hii sio mara ya kwanza kwa msanii wa Bongo Fleva kuhusu figisu figisu za views kwenye mtandao wa YouTube kwani Baraka The Prince alishawahi kukiri kuwa kuna watu wanamfanyia mchezo huo.

Top Post Ad

Below Post Ad