Viongozi 12 Hawajulikani Walipo - Mbunge Mbwege

Viongozi 12 hawajulikani walipo - Mbunge Mbwege
Mbunge wa Kilwa Kusini Selemani Bungara kwa tiketi ya CUF amefunguka na kusema kuwa kuna viongozi kumi na wawili walikamatwa na polisi Rufiji lakini mpaka sasa hawafahamiki viongozi hao wapo wapi na wameshindwa kufikishwa mahakamani.


Bungara amesema hayo bungeni na kusema kuwa atashangazwa sana na wabunge wa CCM hasa wanawake ambao watakuwa wakiiunga mkono na kusema hapa kazi ili hali kuna wanawake wenzao kadhaa wamekamatwa na hawafahamiki mpaka saizi wapo wapi.

"Mhe. Mwigulu kuna viongozi wengine 12 mmewakamata na hawajulikani mpaka sasa wapo wapi, kiongozi wa kwanza ni Ziada Nongwa huyu ni diwani viti maalum kwa tiketi ya CUF na ana mtoto mchanga mmemkamata mmemchukua na hajulikani wapi alipo ni mama huyu hivyo nitaona ajabu sana kina mama wa CCM mama mwenzenu tena diwani kakamatwa na hajulikani alipo halafu mseme hiyo ndiyo kasi, mwingine ni Moshi Mchera Mwenyekiti wa Kitongoji na ni mwanamke pia, Brazili Lyango na mkewe, Jumanne Kirumeke Mwenyekiti wa Ikwiriri, Kisanga Athumani Katibu wa vijana wa CUF, Kasi Mtotela, Mtuko Astela Katibu wa CUF Kata ya Ikwiriri, Khamisi Nyumba Katibu wa CUF wilaya ya Rufiji, Baratu Kisongo, Nanjooma Mlanzi mfanyabiashara Ikwiriri, Abdalah Mkiu na Salimu Mkiu Mwenyekiti mstaafu wa UMWE" alisema Bungara

Mbunge Bungara aliendelea kusisitiza kuwa viongozi wote hao ambao amewataja hapa wamekamatwa na jeshi la polisi lakini hawafahamiki wapi wapo na kusema hawajafikisha mahakamani jambo ambalo ni kinyume na sheria.

"Wote hawa mmewakamata tunaomba mtuambie wapo wapi hawa watu, waleteni mahakamani nakuomba sana Mhe. Mwigulu Nchemba mtuambie hawa watu wako wapi na lini mtawafikisha mahakamani kwani wazee wao wanalia"

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad