Vodacom M-Mpesa Yasherehekea Miaka Kumi ya Kubadilisha Maisha ya Watanzania



Huduma ya Vodacom M-PESA imetimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake mwaka
2008. Katika miaka hiyo, Vodacom M-Pesa imejikita katika kutoa huduma mbalimbali
kama kulipia huduma na bidhaa, huduma za kibenki, kuweka na kukopa pesa,
kutuma pesa nje ya nchi na huduma nyingine nyingi. Huduma hizo zote zinapatikana
kwa njia rahisi sana ya huduma ya pesa kwa njia ya mtandao ambayo ilikuwepo
tangu mwanzoni.

MKurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao (katikati) akifafanua jambo
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam jana, kuhusiana na
maadhimisho ya sherehe ya Miaka 10 ya M-Pesa itakayofanyika Juni 13, 2018,
wakati wa mkutano na waandishi uliofanyika makao makuu ya Kampumi hiyo. Kulia
kwake ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc,
Rosalynn Mworia.
Hadi sasa, Vodacom M-Pesa inaongoza Tanzania kwa huduma za kifedha za
mtandao kwa makampuni ya simu za mkononi kwa asilimia 42 na imeweza kutoa
huduma kwa Watanzania vijijini na mijini ambapo wameweza kutumia huduma halali
ya kifedha na kusababisha kukua kwa uchumi wa Taifa kutoka 58% 2013 na 44%
2009 hadi 65% kwa mwaka 2017.
“Mafanikio ya M-Pesa kwa miaka kumi iliyopita yanamaanisha mwanzo mpya wa
malipo kwa njia ya kidijitali hapa Tanzania. M-Pesa imegusa na kubadilisha maisha
ya mamilioni ya Watanzania pekee. Miaka kumi iliyopita, M-Pesa ilimaanisha kutuma
na kupokea pesa kutoka kwa mteja mmoja kwenda kwa mwingine. Leo hii, M-Pesa

inaamanisha maisha ya kila siku na inaendelea kukua kwa huduma mbali mbali.
Vodacom M-Pesa ndio mtandao pekee hapa Tanzania wenye kutumia huduma za
QR code na hivyo kuongoza kwenye huduma za ziada na nafuu na kuwa teknolojia
inayoongoza kiuwekezaji na sio Tanzania tu bali barani Afrika,” alisema Ferrao.


Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao (kulia) akimkabidhi zawadi
mwandishi wa habari wa EATV, ambaye alikuwepo wakati wa uzinduzi wa huduma
ya M-Pesa 2008, Samweli Njonanje. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na
Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalynn Mworia.

VIDEO:

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad