Wanasiasa watano nchini Australia wamelazimika kujiuzulu kutokana na kugundulika kuwa na uraia wa nchi mbili kipindi ambacho walichanguliwa kushika nafasi hizo.
Mwaka jana, wabunge 10 nchini humo pia walivuliwa ubunge kutokana na kuwa na uraia wa nchi mbili tofauti na katiba inavyohitaji kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi.
Suala la uraia wa nchi mbili linatajwa kuyumbisha Bunge na serikali ya Australia kwa ujumla tangu mwezi July, 2017 na limewahi kuhatarisha baraza la mawaziri.