Wanawake Waandamana Vivua Wazi wakipinga Unyanysaji wa Jinsia

Wanawake Waandamana Vivua Wazi wakipinga Unyanysaji wa Jinsia
Zaidi ya Wanawake 5,000 wameandamana katika mitaa ya mji wa Tel Aviv nchini Israel wengi wao wakiwa vifua wazi wakipinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia bila ya kuvaa kitu katika vifua vyao wakipinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia nchini humo.

Wanawake hao walioshikilia mabango yenye ujumbe tofauti tofauti wameandamana siku mbili kuanzia Mei 5 hadi jana Mei 7, 2018. Ambapo wamesema lengo la maandamano hayo ni kupaza sauti kwenye jamii kuacha vitendo vya  ubakaji na kubadili mfumo wa utoaji haki kwenye mahakama ambao ni kandamizi kwao.

Kwa mujibu wa mtandao wa Russia Today, umeeleza kuwa wanawake hao pia walikuwa wanapinga zuio la kuvaa nguo fupi au zile zinazoacha asilimia kubwa miili yao ikiwa wazi.
‘Not your toy’: 5,000 feminists go on topless SlutWalk in Tel Aviv in spirit of #MeToo
Zuio hilo lilitangazwa mwaka jana na serikali nchini humo kufuatia hashtag ya #MeToo kuanza kutumika kwenye mitandao ya kijamii duniani kote na wanaharakati pamoja na wanawake maarufu duniani wakipinga unyanyasaji wa kijinsia.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad