Watu 27 Wafariki Kutokana na Mvua Zinazoendelea Kunyesha Kenya na Kuvunja Kuta za Bwawa

Watu 27 Wafariki Kutokana na Mvua Zinazoendelea Kunyesha Kenya na Kuvunja Kuta za Bwawa
Watu 32 wamefariki  dunia huku wengine wakikosa mahali pa kuishi baada ya  bwawa la Patel kubomoka kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jana  usiku.

Taarifa kutoka nchini humo zinasema kwamba watu wengi hawafahamiki walipo mpaka sasa.

Bwawa la Patel mjini Nakuru katika mkoa wa bonde la ufa lilibomoboka jana usiku na kusomba mamia ya nyumba za wakazi waliokuwa karibu na eneo hilo.

Waziri wa Mambo ya Ndani Kenya, Fred Matiangi amewasili katika eneo hilo.

Mmoja ya walioshuhudia maafa ya kupasuka kwa bwawa hilo nchini Kenya anasema imeonekana miili iliyofukiwa katika matope.

“Tulipata miili 11 iliyokuwa imefukiwa na matope katika shamba moja la kahawa na hawa ni watu ambao huenda walikuwa wakijaribu kujiokoa  lakini hawakufanikiwa kutokana na nguvu na kasi ya maji ,’’amesema.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi wengi wao ni wawawake na watoto ambao hawakuweza kukimbia kwa kasi pamoja na wazee.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad