Waziri Majaliwa: Imani ya Dini na Maendeleo ya Watu Haviwezi Kutenganishwa

Waziri Majaliwa: Imani ya Dini na Maendeleo ya Watu Haviwezi Kutenganishwa
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa amesema kuwa imani ya dini yoyote ni lazima iendane na maendeleo ya watu ni mambo mawili ambayo hayawezi kutenganishwa kwa maslahi ya Taifa.


Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo jana Mei 20, 2018 Jijini Dodoma katika ibada maalumu ya kumtawaza Askofu Dkt. Maimbo Ndolwa kuwa Askofu mkuu wa kanisa la Anglikana nchini Tanzania na kuongeza kuwa ni jukumu la viongozi wa dini ni kuhimiza waumini kufanyakazi kwa bidii

“Imani ya dini na maendeleo ya watu haviwezi kutenganishwa, kwa maana hiyo hutuwezi kutenganisha imani ya dini na changamoto kubwa zinazotukabili ikiwemo, umaskini, maradhi na ujinga kwa namna nyingine umaskini huletwa na watu kutofanyakazi ni vizuri tuhimize waumini wote kufanyakazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo na kuondoa umaskini”, amesema Majaliwa.

Kwa upande mwingine Waziri Mkuu Majaliwa aliwasisitiza viongozi wa dini nchini kuendelea kuliombea Taifa la Tanzania na viongozi hasa Rasi Dkt John Magufuli ili awe na busara, hekima, upendo na hekima katika kuiletea nchi maendeleo.

Askofu Dkt. Maimbo Ndolwa alitawazwa kuwa Askofu Mkuu wa saba wa kanisa la Anglikana nchini Tanzania katika ibada iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Dayosisi ya Central Tanganyika Jijini Dodoma

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad