Baada ya wachezaji baadhi wa Yanga kutoonekana dimbani kwa muda mrefu, uongozi wa Yanga umesema unahofia kuvunja nao mikataba kwa hofu ya kupata hasara.
Donald Ngoma na Amis Tambwe ni miongoni mwa wachezaji walioshindwa kuichezea timu hiyo kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema kuwa wana hofu ya kuvunja nao mikataba kwasababu itawalazimu kuwalipa fedha za uvunjaji.
Kauli ya Mkwasa imekuja kutokana na klabu hiyo kutokuwa vizuri kiuchumi kwa sasa tangu Mwenyekiti wao Yusuph Manji kutangaza kujiuzulu nafasi yake.
Kutokuwepo kwa wachezaji hao kumechangia kikosi hicho kushindwa kupata matokeo yasiyo mazuri kwenye ligi msimu huu kwani huduma yao ina muhimu mkubwa ndani ya timu.