Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Kabwe amesema kuwa amefurahi kuona Mbunge mwenzake wa Mbeya Mjini kupitia tiketi ya CHADEMA, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu pamoja na mwenzie Emmanuel Masonga wakitoka gerezani lakini amekataa kuwapa pole kwa kile alichodai kuwa viongozi wote wa upinzani kwa sasa ni wafungwa watarajiwa.
Zitto amesema kuwa anaamini kukaa kwao gerezani kumewaongezea zaidi ari ya kupambania Demokrasia pana ya nchi yetu. “Nafurahi kuwa Mbunge Mbeya Mjini Ndg. Joseph Mbilinyi (Sugu) na mdogo wangu Emmanuel Masonga wametoka Gerezani! siwapi pole, maana katika nyakati za Udikteta wapinzani wote ni wafungwa watarajiwa.
Naamini kukaa kwao gerezani kumewaongezea zaidi ari ya kupambania Demokrasia pana ya Nchi yetu.Watawala mjue sasa kuwa vifungo vya Uonevu, kututishia Maisha na hata kutupiga risasi havita turudisha nyuma kwenye kupigania demokrasi ya nchi yetu.“ameandika Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Mhe.
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameachiwa huru leo Mei 10, 2018 kutoka gereza la Ruanda, Mbeya alipokuwa akitumikia kifungo cha miezi mitano kwa makosa ya uchochezi.