JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limeawakamata watu 15 akiwemo Lule Lusale (35) mkazi wa Rgani Ng’ambo na wenzake kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa mitandaoni kwa njia ya kuwatumia watu mbalimbali ujumbe mfupi wa simu wakitaka wawatumie pesa haraka, simu 45, kadi 352 za simu, vitambulisho na komputer mpakato (laptops) zipatazo 5.
Akizungumza na wanahabari, Kamanda wa Oparesheni Maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi, Liberatus Sabas amesema watuhumiwa hao wamekamatwa jijini Dar es Salaam na wengine mkoani Rukwa ambapo baada ya kufanyiwa upelelezi wamekiri kuhusika na matukio ya wizi huo ambao kwa sasa umesambaa mitandaoniu na kusema wamekuwa wakitumia mfumo wa Bulk SMS ambao unawawezesha kutuma jumbe zaidi ya 10,000 kwa wakati mmoja.
“Baada ya lkupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, jeshi letu lilianza uchunguzi na kuwabaini watuhumiwa hao ambao wamekamatwa, walikuwa wakituma jumbe zinazosomeka kama ifuatavyo.
Ujumbe wa kwanza; “Nitumie hiyo hela katika namba hii”, ujumbe wa pili; “Namba ile ya awali ina matatizo, nitumie sasa hiyo hela katika namba hii,” Ujumbe wa tatu; “Namba ile ya wawai ina matatizo, sasa nitumie hivi”, ujumbe wa nne; ” Mganga wa jadi, msamalia, Je, unasumbuliwa na magonjwa sugu, ndoa, pesa na majini? Pete, kusafisha nyota wasiliana na namba 074213……. huduma itakufata popote ulipo” hawa wote walikuwa ni matapeli,” amesema Sabas.