50 Cent Alivyoishangaza Dunia Kwa Kujikondesha Kupita Kiasi ili Acheze Movie...


Moja ya kitu kikubwa ambacho ili entertainment industry yoyote ifanye vizuri ni pale ambapo wahusika watafikia hatua ya kuacha kufanya vitu kwa mazoea na kufanya katika uhalisi zaidi.

Imezoeleka mara nyingi iwe kwenye film au music kunatokeaga kasoro mbalimbali ambazo huwafanya mashabiki kuanza kuzichoka baadhi ya kazi kwa kuona hazijafanyika kwenye kiwango husika na badala yake imefanyika kwa mazoea zaidi.

Mwaka 2011 mwanamuziki maarufu duniani @50cent aliingia kwenye upande wa film na kitu kikubwa cha kujifunza ni jinsi ambavyo aliamua kujikondesha kabisa kwa ajili ya kubeba uhalisia kwenye film iliyojulikana kama ALL THINGS FALL A PART.

Kitu alichokifanya @50cent kilikuwa kinabeba uhalisia wa film hiyo kwa sababu ilikuwa inaonesha kwamba kila kitu alichokuwa anakitegemea maishani alikipoteza na ili kuonesha uhalisia aliona akisema amefilisika halafu anaonekana ana afya uhalisia utapotea akaamua kujikondesha kabisa ili kuonesha uhalisia wa kile kinachoonekana kwenye film hiyo.

JE KWA UPANDE WAKO UNAHISI ENTERTAINMENT INDUSTRY KWA MAANA MUSIC NA FILM HAPA TANZANIA WANAKOSEA WAPI KATIKA UHALISIA WA KAZI ZAO.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad