Msanii mkongwe wa BongoFleva nchini Afande sele ameonywa na rapa Zaiid kuacha kubishana na umma walioupitisha wimbo wake wa 'wowowo' mpaka kufikia hatua ya kutambulika kila mahali kwasababu zake binafsi zisizokuwa na tija.
Hayo yameelezwa na Zaiid wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha 'FNL' inayorushwa mubashara kupitia EATV kila siku ya Ijumaa baada ya mkongwe huyo ku-dis ngoma kuwa sio nzuri na hata Marehemu Baba wa Taifa Julius Nyerere angeamka kutoka kaburini kwake akiikuta inafanya vizuri katika nchi ya Tanzania na mipaka yake basi angesononeshwa na tasnia hiyo nzima.
"Nina muheshimu sana bwana Afande Sele kwasababu ametukuza lakini sasa ajaribu kubishana na wabongo nasio uuma. Umma ndio umeamua kuupitisha huo muziki hata hivyo afande kabla ya wowowo alishasema mimi hanijui kwenye group za hip hop", amesema Zaiid.
Pamoja na hayo, Zaiid ameendelea kwa kusema "najua ni utu uzima nao unamchangia lakini mimi nina muheshimu, ukiachilia Afande kuwa ni msanii pia yeye ni shabiki wa nyimbo zangu maana hata washkaji zangu nilivyotoa wowowo walisema ni wimbo mbaya".
Zaiid aliishia wimbo wa Wowowo mwaka 2017 na kushika kasi na kupendwa na watu wengi mpaka kufikia hatua ya usumbufu kuongezeka kwa msanii huyo baada ya mashabiki wengi na marafiki zake kuomba namba wakihitaji mawowowo yaliyomo kwenye wimbo wake.