Senegal imeungana na mataifa mengine kutoka Barani Afrika kuyaaga mashindano ya kombe la dunia baada ya kukubali kipigo cha bao 1 – 0 kutoka kwa Colombia mchezo wa kundi H.
Senegal imekubali kipigo hicho dakika ya 74 kutoka kwa mchezaji wa Colombia Yerry Mina na kuungana na timu za Tunisia, Nigeria, Morocco, na Misri kuyaaga rasmi mashindano hayo.
Kwenye michezo hiyo ya kundi H Japani imeungana na Colombia kwenda hatua ya 16 bora baada ya kushika nafasi ya pili kwenye msimamo huo kwa kuwa na jumla ya pointi nne.
Kuna kila sababu ya Waafrika kukaachini na kujiuliza hasa sababu zilizochangia timu zao kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano hiyo mikubwa na inayoangaziwa na wendi dunia na kushindwa kutinga hata robo fainali.