Ahukumiwa Miaka 3 Jela kwa Kuwauzia Watu Sambusa za Nyama ya Paka

Ahukumiwa Miaka 3 Jela kwa Kuwauzia Watu Sambusa za Nyama ya Paka
Mtu aliyetuhumiwa kwa kuuza nyama ya paka katika sambusa amehukumwa kifungo cha miaka mitatu na mahakama ya Nakuru

Hakimu mkuu Benard Mararo alimhukumu James Mukangu Kimani baada ya kukiri kosa hilo alipowasili katika mahakama hiyo siku ya Jumatatu.

Bwana Kimani alishtakiwa kwa kuchinja na kuuza nyama ya paka kwa wateja wake mnamo mwezi Juni 24 mjini Nakuru.

Alishtakiwa kwamba alimchinja paka kwa matumizi ya binaadamu kinyume na sheria ya chakula , dawa na kemikali.

Mwanamume huyo alikamatwa Jumapili ambapo inadaiwa alipatikana akimchuna ngozi paka.

Gazeti la Star linasema mwenyewe alikiri kupika sambusa akitumia nyama hiyo.

Taarifa kwenye vyombo vya habari Kenya zinasema mwanamume huyo alikiri kuuza nyama ya paka zaidi ya elfu moja mjini humo tangu mwaka 2012.

Gazeti la Nation linasema aliwaambia wanahabari kwamba alianza 'biashara' hiyo baada ya "kugundua kulikuwa na pengo sokoni".

Alisema huwa anauza pia ngozi za paka na kwamba kwa kila paka hujipatia takriban Sh500 (Dola 5 za Marekani).

"Huwa nawaambia wateja wangu kwamba huwa naipata nyama hii kutoka Gioto (jaa la kutupa taka), lakini huwa hawajui kwamba ni nyama ya paka," alinukuliwa na gazeti la Nation.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad