Aishi Manula Naye Awekwa Kando Michuano ya Kagame

Aishi Manula Naye Awekwa Kando Michuano ya Kagame
Kipa Aishi Manula hataichezea Simba katika michuano ya Kombe la Kagame.

Simba imeamua kumuweka Manula katika listi ya wachezaji wanaopumzishwa wakati wa michuano hiyo itakayofanyika mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es Salaam.

Manula ndiye kipa aliyedaka mechi nyingi zaidi kwa msimu uliopita kwa kuwa alishiriki michuano mingi akiwa na Simba.

Nafasi ya Manula itachukuliwa na Said Mohammed 'Nduda' ambaye alidaka mechi mbili tu za ligi kuu kutokana na kuandamwa na majeraha.

Pamoja na Manula, Simba imewapumzisha wachezaji wake zaidi akiwemo Haruna Niyonzima ambaye ni majeruhi.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad