Akon Kutoa Sarafu Yenye Jina Lake Senegal

Akon Kutoa Sarafu Yenye Jina Lake Senegal
Akon anasema kuwa anapanga kutoa sarafu ilio na jina lake itakayoitwa Akoin.

Akizungumza katika tamasha la Cannes Lions siku ya Jumatatu , mwimbaji huyo amesema kuwa anaamini kwamba sarafu hiyo ya kidijitali huenda ikaiokoa Afrika.

Tovuti rasmi ya Akoin inasema kuwa msanii huyo anataka programu hiyo kuweka katika kila simu ya rununu kati ya sasa na mwezi Disemba.

Na Akon anasema kuwa anapanga kujenga mji wa kidijitali nchini Senegal utakaokuwa na 'hali halisi ya Wakanda'.

Tovuti hiyo imefaidika na ekari 2000 za ardhi kutoka kwa rais wa Senegal ili kujenga mji huo - ambao ameutaja jina lake.

Ameutaja kuwa mji wa kidijitali asilimia 100 huku sarafu ya kidijitali ikutumika kufanya biashara.

Chini ya mazingira ya sarafu ya kidijitali ya Akoin, wateja wataweza kununua , kuhifadhi na kutumia sarafu hiyo moja kwa moja kutoka kwa simu zao za rununu.

''Inarudisha uwezo kwa raia na kurudisha usalama katika mazingira ya sarafu hiyo'', Akon alielezea.

''Pia inawaruhusu watu kuitumia kwa njia ambayo wanaweza kujiendeleza na kutoruhusu serikali kufanya mambo yanayoakwamisha maenedeleo''.

Hatahivyo Akon amekiri kwamba hajui maswala ya kiufundi ya uwekezaji huo mpya.

''Nilikuja na mradi huu hivyobasi nataka magwiji kuketi chini na kuona utakavyofanyika'', alisema.


Inatumia habari katika kodi ambayo haiwezi kutambulika kwa urahisi ili kufanyia biashara. Hatua hiyo inaifanya kuwa vigumu kutengeza sarafu bandia.

Sarafu ya kwanza ya kidijitali ni Bitcoin ambayo ilianzishwa na mtu asiyejulikana kwa jina Satoshi Nakamoto mwaka 2009.

Baadhi ya watu maarufu wameunga mkono na kuwekeza katika fedha za kidijitali kama vile Katy Perry, 50 Cent na Ashton Kutcher.

Top Post Ad

Below Post Ad