Alikiba, Samatta Kuonyeshana Ubabe Taifa Leo

Alikiba, Samatta Kuonyeshana Ubabe Taifa Leo
BAADA ya Ally Salehe Kiba ‘Alikiba’ kutamba timu yake itaibuka na ushindi mbele ya timu ya Samatta, mwenyewe ameibuka na kumjibu mpinzani wake.



Mbwana Samatta ambaye anai­chezea KRC Genk ya Ubelgiji, ameunda timu yake ambayo leo Juma­mosi ina­tarajiwa kucheza mechi maalum na timu ya Alikiba katika Uwanja wa Taifa, Dar ikiwa na lengo la kuchangia elimu hapa

Tanzania.

Akizungumza na waandi­shi wa habari, Samatta al­isema anaamini wachezaji aliowachagua kuunda timu yake watampa matokeo mazuri katika mchezo huo.



“Tumejipanga kufanya vizuri kwani tumefanya maandalizi ya kutosha kwa upande wetu tayari kwa mchezo huo, nawaamini wachezaji niliowachagua tutafanya vizuri.



“Kama inavyofahamika ni kwamba lengo la mchezo huu ni kuchangia elimu na wazo hili lilikuwa ni langu, nikaona bora nimshirikishe mwenzangu Alikiba.



“Huu ni mwanzo tu, malengo yetu ni kuona hili jambo linakuwa endelevu kwa nchi nzima na si Dar pekee,” alisema Samatta.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad