AS ROMA Yashindwa Kuficha Hisia Zake kwa Nigeria

AS ROMA Yashindwa Kuficha Hisia Zake kwa Nigeria
Hapo jana usiku timu ya taifa ya Nigeria iliyaaga mashindano ya michuano ya kombe la dunia nchini Urusi baada ya kutolewa na Argentina kwa jumla ya mabao 2 – 1 matokeo yaliyoacha simanzi kwa Waafrika na hata wasiyo wa bara hilo waliyokuwa na mapenzi mema na The Super Eagles.



Kabla hata ya michuano hiiyo kuanza klabu ya AS ROMA ya Italia ilionyesha mapenzi yake ya wazi dhidi ya miamba hiyo ya Afrika na kuitabiria makubwa kwenye kombe hilo.

Baada ya kutolewa na Argentina klabu ya AS ROMA kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter imeandika ujumbe kuwa inajiskia vibaya kupata matokeo mabaya Super Eagles.

Ni huzuni, hii ni kwa wote Super Eagle na mashabiki wake wenye hisia, ilikuwa na jezi nzuri zaidi, kupitia Nigeria tumetengeneza marafiki wengi zaidi wapo watakao baki nasi na wapo ambao wataondoka lakini tunaimani ipo siku moja tutaonana Roma ama kuwatembelea Lagosi.



Kabla ya mechi ya Nigeria dhidi ya Argentina AS Roma iliibashiria The Super Eagle kushinda kwa asilimia 44.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad