Askofu Akamatwa kwa Utapeli Dodoma

Askofu Akamatwa kwa Utapeli Dodoma
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia Askofu Martin Gwila wa Kanisa la Agape Sanctuary International kwa tuhuma za utapeli wa kiasi cha zaidi ya Sh 63 milioni.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema kiasi hicho cha fedha alikipata baada ya kuwadanganya watu mbalimbali kuwa atawapa ajira kupitia kanisa lake.

Pia anadaiwa kuwalaghai waumini akiwataka watoe fedha ili wasajiliwe na alitoza viwango tofauti vya fedha.

“Askofu huyo alikamatwa mwishoni  mwa  wiki jijini Dodoma na alipokea fedha hizo pasipo kutoa ajira yoyote huku akitoa vitisho kwa waliotoa fedha hizo,” alisema

Kamanda Muroto  amesema kuwa kanisa hilo ambalo makao yake makuu yapo Arusha halijasajiliwa kwa mujibu wa sheria kama kanisa bali aliisajili Agape Sanctuary kama kampuni binafsi.

Mtuhumiwa atafikishwa mahakani muda wowote kuanzia sasa.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad