Auawa masaa machache kabla ya harusi


Binti Oyinye Aguluka ameuawa kwa kukatwa na panga na baba yake mzazi, Cletus Aguluka, masaa machache kabla ya harusi yake.

Binti huyo ambaye anaishi nchini Nigeria yalimkuta masahibu hayo akiwa amelala usingizini, baada ya baba yake aliyekuwa amelewa kuja na panga na kumshambulia.

Mama Mzazi wa marehemu aliyetambulika kwa jina la  Georgina  amesema mume wake alirudi usiku akiwa amelewa na kuwauliza watoto wake mahali ilipo tochi yake, lakini hakuna ambaye alimjibu kutokana na kwamba walikuwa wameshaingia kulala, na ndipo alipokuja na panga na kuanza kumshambulia binti yake huyo ambaye alitakiwa kufunga ndoa Jumamosi hii ya Juni 2, 2018.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa na wazee wa kijiji na kupelekwa kituo cha polisi, ambako anashikiliwa mpaka sasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad