Chama cha wakulima Tandahimba (Tandahimba Farmers Association -TAFA) walikutana na Waandishi wa habari Dodoma na kutoa msimamo wao juu ya mjadala ulioibuka bungeni kuhusu fedha za ushuru wa mauzo ya korosho ghafi nje (export levies) ambapo wametaka ushuru wa 65% kuendelea kupelekwa kwenye sekta moja kwa moja bila ya kupitia Serikali kuu.
“Hoja kubwa ya wadau ni kwamba fedha hii ikipitia Serikali kuu mambo mengi hayatatekelezwa lakini pia kwa sababu ya changamoto zilizopo za utekelezaji wa bajeti itakuwa vigumu kusimamia fedha hizo zikiwa kwenye mfuko wa Serikali”-M/Kiti Mohamed Jabuka
Baada ya Hoja ya Korosho Kuwavuruga Wabunge Huu Hapa Msimamo wa Wakulima wa Zao Hilo
June 26, 2018
Tags