Babu Tale Asimulia Alivyowaonya Daimond na Hamissa Mobetto "Zari Sio Adui Yako Kama Unataka Kumkomesha Kamkomeshe Lulu"

Babu Tale Asimulia Alivyowaonya Daimond na Hamissa Mobetto "Zari Sio Adui Yako Kama Unataka Kumkomesha Kamkomeshe Lulu"
Drama bado haziishi kwa upande wa Diamond Platnumz na Hamisa Mobetto.

Kwa sasa meneja wa Diamond, Babu Tale amesema kabla ya Hamisa kuzaa na Diamond alishawaonya kwani wakati huo Diamond alikuwa katika mahusiano na Zari.

“Kabla Hamisa hajapata ujauzito, tulikuwa tuna-shoot video ya Salome nikamwambia Zari sio adui yako, kama una mapenzi na Diamond mpende ila kama unataka kumkomesha, kamkomeshe Lulu, ila kama unataka kufanya hivyo haipendezi,” amesema.

“Nikamwambia pia Diamond kama unafanya ujana, inatakiwa pia uangalie ujana wako yule demu (Zari) amekuja huko from nowhere amekuzalia mtoto pia,” Tale ameiambia Wasafi TV.

Moja ya sababu alizoeleza Zari kuwa zilichangia kuachana na Diamond Platnumz ni kitendo cha kuzaa na Hamisa Mobetto. Babu Tale kwa sasa yupo nchini Afrika Kusini kuhakikisha Diamond na Zari wanamaliza tofauti zao.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hakuna mtu muongo na mnafiki kama babu tale.

    ReplyDelete
  2. Babu wacha unafiki zee zimaa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad