Bad News: Kichanga cha Miezi Sita Chateketea kwa Moto Kilimanjaro

Bad News: Kichanga cha Miezi Sita  Chateketea kwa Moto Kilimanjaro
Mtoto wa miezi sita, amefariki dunia baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi, kuteketea kwa moto asubuhi ya leo katika eneo la Njia Panda ya Himo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo leo Juni 6.

Kamanda Issah amesema, tukio hilo limetokea leo saa 3 asubuhi, wakati mama wa mtoto huyo, akipika vitumbua nje.

“Ni kweli kuna moto umetokea Njiapanda ya Himo na kusababisha kifo cha mtoto wa miezi sita, polisi tunaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo,”amesema Kamanda Issah.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad