Padri Mwimba Rap Asimamishwa Kazi

Kasisi mmoja wa kanisa Katoliki nchini Kenya aliyepata umaarufu kutokana na mtindo wake wa kutumbuiza kwa kutumia muziki wa kufoka amesimamishwa kazi.

Paul Ogalo aka 'Sweet Paul' amekuwa akitumia muziki wa rap kama njia ya kuwavutia vijana wengi kufika kanisani.

Alikuwa amesema muziki ni njia mwafaka sio tu kuwavutia vijana bali pia kueneza Injili.

Mistari ya nyimbo zake huwa kwa mfano: "Kujeni church kuna baraka, kujeni church kuna baraka..." au "Father Paul, niki-lock kwenye mic, Nduru inafuata, mamanze go tipsy, vijana ruka ruka swag ya kunguru, au sio"

Lakini hatua yake hiyo inaonekana kutowafurahisha viongozi wa kanisa Katoliki magharibi mwa Kenya ambao wamemsimamisha kazi kwa mwaka mmoja ili "ajitafakari".

Askofu wa jimbo la kanisa Katoliki la Homa Bay Philip Anyolo amesema padri huyo ni lazima achague kati ya kuwa „rapa na kuwa padri".

Amesema kasisi huyo hataruhusiwa kuongoza ibada ya misa kwa kipindi cha mwaka mmoja ingawa anaruhusiwa kushiriki ibada, na pia anaruhusiwa kufanya ibada ya misa lakini faraghani.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad