BAKWATA yapiga marufuku kutangaza Eid


Baraza Kuu la waislam Tanzania (BAKWATA) limepiga marufuku utangazaji wa sherehe za Iddi na sherehe zozote zile za dini ya Kiislam bila kupata vibali vya baraza hilo ambalo ndio chombo kikuu cha kusimamia dini hiyo nchini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Taifa BAKWATA na Msemaji Mkuu wa Mufti Mkuu Tanzania, Sheikh Khamis Mataka mbapo amesema kumekuwa na mkanganyiko wa siku na tarehe za sikukuu za Iddi kutokana na baadhi ya watu kujiamulia kutangaza bila kuwa na vibali vya dini hiyo hali ambayo imekua inaleta shida kwa waumini wa dini hiyo.

"Kufuatilia na kutangaza mwezi mwandamo ni suala muhimu na lenye kupewa uzito mkubwa sana na dunia kote jambo hilo huwa kuna mamlaka maalum ambayo inautangaza huo mwezi baada ya  kuuthibitisha", amesema Mataka

Pamoja na hayo, Sheikh Mataka ameendelea kwa kusema "leo Alhamisi Juni 14 ndio tarehe 29 Ramadhani na magharibi yake mwezi ufuatiliwa ili kama umeandama inatangazwa Eid Al Fitr".

Kwa upande mwingine,  Sheikh Mataka amewaomba umma wa kiislamu endapo watafanikiwa kuuona mwezi muandamo basi watoe taarifa kwa sheikh wake au Imam wa msikiti  ili mamlaka zinazohusika na kuutangaza ziweze kuujuza umma.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad