Balozi wa Syira nchini Abdulmonem Annan ameiomba radhi serikali ya Tanzania baada ya kusambaa kwa video iliyomuonyesha akisema atahamasisha raia wa Syria, wasiwekeze nchini kwa kile alichodai polisi hawalifanyii kazi suala la kuporwa fedha kwa Ofisa Ubalozi wa Syria.
Machi 20, Ofisa Ubalozi huyo, Hassan Alfaouri alishambuliwa na watu wasiojulikana na kuporwa zaidi ya euro 9300(zaidi ya Sh 25 milioni).
Baada ya tukio hilo, Balozi huyo alisema alitoa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwa njia ya video akisema kuna ufuatiliaji hafifu wa suala hilo na hivyo atahamasisha raia wa Syria wasije kuwekeza nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Suleman Salehe alisema maneno aliyosema balozi Annam yalikuwa ni ya uchochezi hivyo waliamua kufanya nae mikutano minne.
Alisema wao kama Wizara walifanya jitihada na kuhakikisha jeshi la polisi linafanya uchunguzi na kuhusiana na tukio hilo na kuwakamata watu wawili ambao ni dereva na katibu wake.
“Wizara inamshukuru Balozi kufunguka na kutoa taarifa muhimu kuwa ametaarifiwa na jeshi la polisi kuwa watuhumiwa wawili wamekamatwa na sehemu ya kiasii cha fedha kimepatikana”amesema Salehe
Amesema kwa kuwa balozi amebakiza miezi michache amalize muda wake hapa nchini, Wizara itaanda taarifa ili aweze kukutana na Mkuu wa jeshi la polisi na washughulikie suala hilo.