Baraka Da Prince Haniwezi Anarudia Maneno Verse Fupi - Golden D

Baraka Da Prince haniwezi anarudia maneno Verse Fupi - Golden D
Msanii Chipukizi wa Bongo fleva Idris Ramadhan, a.k.a Golden D, amesema kuwa watu wengi wamekuw wakimfananisha na diamond platnumz, ana inabid akubai kwasababu ni watu ndivyo wanavyosema hana budi kukubali, na kusema kuwa pamoja na hayo kazi yake ya kwanza ambayo inaitwa sangida, ameifanya katika studio za WCB, na amesekuwa kuwa kuna kolabo inakuja na Rayvanny.

Vilevile msanii huyo chipukizi amedai kuwa kuna wasanii ambao wanatakiwa kuwa makini na yeye na anaweza kuwakalisha chini kutokana na kuona hawamuwezi ila waliwahi kupata jina ambapo aliwataja wasanii watatu akiwemo, Baraka Da Prince, Marioo, Beka Flavour na kutaka wajipange kwania na aweka mziki sawa.

"Kiukweli mimi wasanii ambao na wapa onyo, nakuja kama radi na kasi sio poa, kuna Marioo, Beka fleva Pamoja na baraka da prince, wale ni wasanii nawaambia wanipe njia nakuja kama fagio kuja kuweka sawa mziki kuupangilia vizuri ili mziki uende kwenye nafasi yake" Golden D amesema

"Baraka the prince ana ka verse kafupi halafu anapenda kurudia maneno na hivyo ndio vitu vya kuja kubalishha" aliendelea kusisitiza
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad