Barnaba Kuachia Albamu Yake Yenye Nyimbo 18 Mwezi Ujao

Barnaba  Kutoa Albamu Yake Mwezi Ujao
Msanii wa Bongo Flava, Barnaba ameweka wazi kuwa amekamilisha albamu yake ambayo inatarajiwa kutoka mwezi ujao.

Albamu ya muimbaji huyo ambayo inakwenda kwa jina la Gold itakuwa na nyimbo zipatazo 18. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ndipo ameeleza kukamilika kwa albamu hiyo.

“Narudia tena kusema hii ni Gold na mgodi umebeba dhaabu ambazo zimepikwa muda mrefu sana, sitaki kusema mengi I can’t wait kwa kweli,” amesema Barnaba.

Awali albamu hiyo ilipangwa kutoka February 2018 lakini ikahairishwa hadi July 2018 kutokana na kile Barnaba alichoeleza kuwa wadhamini wake wakuu watatu walipendelea hivyo.

Mwanzoni mwa mwaka huu katika kipindi cha The Playlist, Times Fm, Barnaba alisema albamu hiyo itakutanisha wasanii wengine kutoka Kenya Uganda na Nigeria.

Wasanii waliotajwa kuwepo katika albamu hiyo ni pamoja na Juliana Kanyomozi na Jose Chameleon kutoka Uganda. Kutoka Bongo kuna Vanessa Mdee, G Nako, Ben Pol, Aslay, Barakah The Prince, Linex na Joh Makini.

Top Post Ad

Below Post Ad