Wimbo huo ambao unasemekana kuwa hauna maadili na umekuwa kama wa kupotosha fikra za jamii ulifungiwa kutosambazwa wala kupigwa eneo lolote lile mpaka utakapo badilishwa lakini msanii mwenyewe anasema kuwa baraza wamezoea kuwaburuza na kuwaonea wasanii hivyo yeye hatokubali kuonewa.
Akijibu na kuelezea kwanini wimbo huo umefungiwa , katibu wa BASATA Godfrey Mngerza amefunguka na kusema kuwa kama Baraza hawa angalii wimbo umetolewa na nani bali wanaangalia kama msanii huyo amefuata taratibu za utoaji nyimbo.
Sisi hatuamngalii huyo ni nani au anafanya nini , sisi tunaangalia tu kama anafanya kazi yak ya sana vizuri,ni kazi ya sanaa na imetolewa na mwanamuziki bila kujali hizo nanii zingine..kwaio baraza la sanaa la taifa linaangalia kazi ya sanaa linaangalia kazi za msanii, lakini pia hatuangalii kazi hii imetolewa official au vipi sisi hilo hatuangalii. sisi kama baraza tunajua kuwa kama kazi haukufuata utaratibu na sio lazima tukukufungia na wala hatuna haja ya kukuita wewe msanii.