Aidha pia ajali hiyo ilisababisha majeruhi kwa watu kumi (10), wanaume sita (6) na wanawake wa nne (4), wote wapo katika hospitali ya Bukumbi wakiendelea kupatiwa matibabu.
Aidha kati ya hao majeruhi mahututi wapo watatu ambao ni Idd Omary, miaka 40, dereva wa gari lililopata ajali, Ibula Raphael, miaka 34, msukuma, mkulima na mkazi wa Busolwa na Sophia Lugihila miaka 45, msukuma, mkulima na mkazi wa msalala na wote wamepelekwa hospitali ya Sekouture iliyoko Mwanza kwa matibabu zaidi.
Chanzo cha ajali ni kuferi kwa breki za gari hali iliyopelekea gari hilo kugonga ofisi za ferry na kusababisha kifo na majeruhi.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Bukumbi kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Kamishina msaidizi wa polisi Mkadamu Khamisi Mkadamu anatoa pole kwa wote hususani kwa ndugu na jamaa wa marehemu wa ajali hiyo, tunawaombea kwa mwenyezi mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu. Aidha pia tunawaombea majeruhi wapone haraka ili waweze kuendelea na kazi.