Baunsa wa Daimond Mwarabu Fighter Aacha Deni Kubwa Sehemu Aliyofanyia Birthday Yake Hadi Leo Ataki Kulipa

Baunsa wa Daimond Mwarabu Fighter Aacha Deni Kubwa Sehemu Aliyofanyia Birthday Yake Hadi Leo Ataki Kulipa
Kama mfatiliaji mkubwa wa story za mastaa utakumbuka ile birthday ya Mwarabu Fighter ambaye ni board gurd wa Daimond sasa leo nakulete ubuyu moto kuhusiana na ishu nzima kumbe anadaiwa mamilioni ya hela ajalipa.

Mwanamuziki wa Muda mrefu Zolla D ambaye ni rafiki wa karibu na Mwarabu amesema kuwa Hana ugomvi na Baunsa wa DIAMONDPLATNUMZ Mwarabu Fighter ila anadaiwa Hela ya matumizi ya  siku ya kuzaliwa ambapo alikubaliana na watu wa chakula, eneo aliyofanyia sherehe yake pamoja na swemming pool ambapo adi sasa anadaiwa na hataki kulipa.

"Mimi ndio nilimconect na hao watu na wao wananisumbua mimi lakini nikimpigia mwarabu akawa ananambia nimsubirie akaja usiku nikamwambia kwanini ajawalipa akasema pesa aliyonayo aitoshelezi ana laki tatu tu akashindwa kumalizana nao wale watu wakataka kumpeleka polisi" Zola

 "Hadi sasa mwarabu ananikimbia na simu yangu apokei nina miezi miwili sina mawasiliano naye sina bifu naye yoyote ila mwarabu anadaiwa hela ya watu pale ofisini kwangu na amekimbia ninachomwambia hata kama hela ndogo anachotakiwa alipe mimi ni mwalimu wake niliyekuwa namfundisha mazoezi lakini hadi sasa haji kwakuwa anadaiwa milioni mbili"

Zolla D alisema watu wengi walimshauri amwambie boss wa mwarabu ambaye ni Daimond lakini kutokana na heshima aliyonayo kwa daimond na ishu yenyewe ni ndogo akuona haja ya kufanya hivyo ila alimtaka Mwarabu Fighter kulipa Deni analodaiwa.

"Watu waliniambia nimwambieboss wake ambaye ni  Daimond nikaona Daimond ni mdogo wangu ambaye ninaheshimiana naye sana siwezi kumwambia jambo dogo kama hili ila kinachotakiwa mwarabu afate sheria alipe hela tu"

Top Post Ad

Below Post Ad