Bibi wa Miaka 65 na Mjukuu Wake Wateketea kwa Moto

Bibi wa Miaka 65 na Mjukuu Wake Wateketea kwa Moto
Bibi wa miaka 65 na mjukuu wake wa miaka mitano mkazi wa kitongoji cha Nga'ang'ati kijiji cha Upper Kitete wilaya ya Karatu mkoani Arusha  wamefariki dunia baada ya nyumba yao  kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.

Akizungumza kwa njia ya simu  na MUUNGWANA BLOG Mwenyekiti wa kijiji ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama ya kijiji hicho  Paskal Paulo amemtaja Kikongwe huyo aliepoteza maisha kuwa ni Scolastica Bura na mjukuu wake aliemtaja jina moja la Chaguzi pamoja na Mbuzi wawili na kondoo mmoja.

Hata hivyo viongozi wa kijiji hicho kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kuuzima moto huo ulieteketeza kabisa nyumba hiyo iliyokuwa imeezekwa kwa nyasi.
Mpaka sasa jeshi la polisi wapo njiani kuelekea katika eneo la tukio takribani kilomita 30 kutoka karatu mjini.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad