Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) leo Alhamisi Juni 7, 2018 inakutana na bodi na menejimenti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuihoji juu ya tuhuma zinazowakabili.
Benki hiyo inatuhumiwa kutumia bima binafsi badala ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Akizungumza na MCL Digital leo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, mwenyekiti wa PAC Naghenjwa Kaboyoka amesema watakutana na BoT leo.
“Leo tumewaita na tutakutana nao. Baada ya kukutana nao taarifa tutaiwasilisha kwa Spika kama alivyotuagiza," amesema Kaboyoka ambaye pia ni mbunge wa Same Mashariki (Chadema)
Tuhuma kuhusu BoT ziliibuliwa na mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga Juni 4, 2018 bungeni katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango mwaka 2018/19.
Amlinga amesema BoT inatumia Sh12bilioni kwa mwaka badala ya Sh1bilioni kugharamia matibabu ya watumishi wake.