Breaking News: Mbunge Prof Maji Marefu Akimbizwa Muhimbili kwa Ndege ya Dharura

Breaking News: Mbunge Prof Majimarefu Akimbizwa Muhimbili kwa Ndege ya Dharura
Mbunge wa Korogwe Vijijini mkoani Tanga Steven Ngonyani  maarufu kwa  jina la Prof Maji Marefu (CCM) ambaye hivi karibuni alipata pigo la kufiwa na mke wake leo hii amesafirishwa kwa ndege ya dharura kutokea mkoani Dodoma kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Bado haijajulikana ni ugonjwa gani ambao unamsumbua Mbunge huyo huku taarifa zikieleza kuwa alikuwa amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma toka Jumatatu ya wiki hii.

Top Post Ad

Below Post Ad