Breaking News: Wananchi 35 watiwa mbaroni kwa kuchoma moto gari la abiria

Na James Timber, Mwanza
Wananchi 35 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa kosa la kuchoma gari la abiria aina ya Isuzu yenye namba usajili  T 257 BJX baada ya kugonga wanafunzi wawili na kusababisha kifo cha mmoja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amesema kuwa tukio hilo limetokea Kata ya Bugogwa wilayani Ilemela Majira ya saa 1:40 asubuhi barabara ya Igombe amesema ajali hiyo ni dereva kutokuwa mwangalifu.

"Chanzo cha ajali hiyo ni wanafunzi walikuwa wanaenda shule wakavuka barabara ndipo walipogogwa na kusababisha kifo cha Naomi Opiyo mwenye umri wa miaka 12, wa darasa la nne na majeruhi kwa mwenzake Burton Opiyo wote wanafunzi wa Shule ya Msingi Kisundi," alisema Msangi.

Kamanda alisema kuwa baada ya ajali hiyo dereva alikimbia na wananchi wakawasha moto gari hilo ambapo ni kinyume na taratibu kwani walianza kufanya shambulio kwa mwananchi aliyewakataka wasijichukulie sharia mkononi na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili.

Aidha Kamanda ametoa onyo kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani atakayebainika anafanya vitendo hivyo atatiwa nguvuni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad